Ubovu wa stendi ya Mabasi Njombe yazua kizaazaa

Posted on

Madereva na watumiaji wa mabasi katika stendi ya mkoa wa Njombe wameiomba halmashauri ya mji huo kukarabati barabara zinazoelekea vijijini kutokana na kuharibika baada ya mvua kubwa kunyesha
Wakizungumza na mwandishi wetu madereva hao wamedai kuwa barabara nyingi zinazoelekea vijijini zimeharibika kitendo kinachopelekea kuchelewa kufika safari zao na hivyo kuonekana ni usumbufu kwa wateja wao ambao ni abiria
Nao baadhi ya abiria wamesema ubovu wa barabara hizo huwalazimu muda mwingine kushuka katika magari na kutembea kwa miguu
Ibrahimu Mkangala ni Mhandisi wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye amewataka watumiaji wa vyombo vya usafiri kuwa wavumilivu kwani halmashauri hiyo tayari imeshapanga mikakati ya kukarabati barabara hizo zilizoharibika mara tu mvua zitakapokwisha
Katika hatua nyingine mhandisi huyo ametolea ufafanuzi ukarabati wa stendi hiyo ya muda ya mabasi mkoani Njombe

from Blogger http://ift.tt/2nwl2WG
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2nA7XwF
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nSquXe
via IFTTT

Leave a comment