VITU 9 AMBAVYO HUTAKIWI KUSHARE NA MTU MWINGINE

Kuna upendo katika kushirikiana vitu lakini kuna wakati upendo huo wa kushirikiana kila kitu unaweza kukuweka katika hali ya hatari sana.

Inapokuwa wakati wa kushirikiana baadhi ya vitu na mtu mwingine, ni vyema ukafikiri mara mbili kabla ya kukubali kufanya hivyo, kwa sababu kukataa ndio jibu unalotakiwa kulisema.

Hapa chini ni orodha ya vitu tisa ambavyo hutakiwi kushirikiana na mtu mwingine yeyote.

1. Sabuni ya kuogea

Watu wengi hawajui kuwa kushirikiana sabuni na mtu mwingine ni jambo la hatari. Mwingine ataamua kutumia sabani ambayo si ya kwake kwa sababu tu anaona uvuvi kwenda dukani kununua ya kwake.

Sabuni inatakiwa kutumia na mtu mmoja kusafishia mwili wake kwani kila mtu ana namna yake ya kutumia sabuni, hivyo haushauriwi kutumia sabuni na mtu/watu wengine.


Uwepo wa vitu kama fangasi au bakteria au wadudu wengine wanaweza kujihifadhi kwenye sabuni na kusababisha maambukizi kwa watu wengine watakaoitumia.

2. Taulo

Hili ni jambo ambalo watu wengi hasa wapenzi au wanandoa hulichukulia kama la kawaida bila kujali kuwa linaweza kuwaletea madhara kiafya.

Kutumia taulo moja mtu zaidi ya mmoja kunaweza kukusababishia madhara mbalimbali kwani kwenye taulo kunaweza kuwepo bakteria mbalimbali.

Mbali na kutumia mataulo tofauti, mnashauriwa kutoyachanganya sehemu moja baada ya kutumia.


3. Mswaki

Ukikaa na kufikiri, unaweza usielewe kwanini mtu anakubali kutumia mswaki wake na mtu mwingine. Licha ya kuwa hili ni jambo la ajabu, lakini hutokea mara nyingi.

Kama ilivyokuwa kwa sabuni, mdomo huwa na bakteria ambapo baada ya kusafisha hubaki kwenye mswaki. Kila mmoja akiacha bakteria wake kwenye mswaki, huenda mkaambukizana matatizo ya kinywa au hata kulika meno.

Lakini wakati mwingine mmoja wenu anaweza kuwa na tatizo la kutokwa na damu kwenye fizi wakati wa kuswaki, kitu kinachosababisha hatari zaidi kwa mwenzake.

4. Hereni

Hereni hasa zile ambazo zinahusisha kutoboa masikio ni hatari sana kwani huwa zina ncha upande wa kuingizia na hivyo kuweza kumchubua mtumiaji wa kwanza na kusababisha maamuziki kwa mtu mwingine kwa kutumia damu iliyotoka wakati ulipochubuliwa.

Kuna wakati mwingine kutokana na gharama kuwa kubwa anashindwa kununua hereni zake anaamua kumuazima rafiki yake, lakini jiulize, huo urembo wa muda ni muhimu kuliko afya yako?


5. Mafuta ya kujipaka

Vidole vya binadamu ni moja ya maeneo ambapo virusi (germs) vinaweza kukaa kutoka na vitu mbalimbali ambavyo huwa tunashika bila kusafisha mikono.

Mtu yeyote anayekuja na kutumbukiza vidole vyake kwenye kopo lako la mafuta kwa nia ya kujipaka, huacha virusi ambavyo mwisho wa siku husambaa kwenye kopo lote. Hii itakufanya ikijakupika wewe, kuweka virusi kwenye ngozi yako.

Bakteria wanaofahamika kama, streptococcus au staphylococcus husababisha kuungua kwa vinyoleo na pia huleta chunusi kutokana na kutumia mafuta na mtu mwingine.

Njia salama ya kutumia mafuta hayo ni kuhakikisha kuwa kunakuwapo na chombo kingine cha kutolea mafuta kwenye kopo, au mafuta unayamimina mkononi. Lakini kwanini uteseke kwa hayo yote? Ni bora kila mmoja akawa na ya kwake.

7. Lip balm

Midomo ya binadamu huwa na mishipa mingi ya damu ambayo kuna wakati mtu anaweza akawa anatokwa damu kwa sababu mbalimbali. Wengine midomo yao hukauka kiasi kwamba inakuwa kama imepasuka.

Katika hali hiyo ni hatari sana kutumia lip balm na mtu mwingine kwani unaweza kumuambukiza magonjwa mbalimbali.


8. Wembe/’Nail clipper’

Ni vigumu kudhani kuwa kuna watu bado hawajui hatari ya kushirikiana kutumia wembe mmoja katika karne hii ya 21. Lakini ukweli utabaki pale pale kuwa kushirikiana kutumia wembe ni kitu cha hatari sana kwa afya yako.

Ni rahisi sana kwa virusi na bakteria kujikusanya kwenye wembe uliotumiwa na mtu mmoja na kisha kumwathiri mwingine atakayeutumia.

Hali hii inakuwa ni mbaya zaidi hasa pale ambapo unatumia wembe na mtu ambaye anaishi na Virusi vya UKIMWI kwa sababu utakuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo.

Licha ya kuwa nail clippers si hatari kama ilivyo wembe, lakini haushauriwi kutumia na mtu mwingine.


9. Spika za masikioni

Inanisikitisha sana kama mimi ndio nitakuwa nakukumbusha au kukwambia kwa mara ya kwanza kwamba kutumia earphones na mtu mwingine ni hatari sana.

Tafiti zimeonyesha kuwa spika za masikioni hubeba bakteria kutoka kwenye masikio ya mtumiaji mmoja kwenda kwa mtumiaji mwingine.

Bakteria kama staph na strep zinaweza kukaa kwenye spika za masikioni na kuhamia kwa mtu mwingine mara tu anapozitumia na kusababisha madhara.

Njia bora ya kutumia spika hizo na mtu mwingine ni kama mtumiaji wa kwanza akimaliza ataziosha vizuri kwa kemikali na kuua bakteria wote, lakini kama hilo haliwezekani, sema hapana kwa yeyote anayetaka kutumia spika hizo kupata mdundo.

Related Posts

Post a Comment