Kijana wa miaka 22 afariki dunia baada ya kuzama mtoni

Kijana mmoja anaetambulika kwa Jina la Suleiman Mtumwa Suleiman mwenye umri wa miaka 22 amefariki dunia baada ya kuzama katika Mto wa Faki Abuu hapo jana huko kilombero Wilaya ya kaskazini B.
Wakizungumza na mwanahabari wetu baadhi ya mashuhuda katika tukio hilo Hija Ali Hija na Habiba Mohamed wamesema tukio hilo limetoka jana majira ya saa 11 jioni na jitihada za uwokozi zilifanyika lakini alishindikana kupatikana hadi leo baada ya kikosi cha uwokozi kufika katika tukio hilo.
Kwaupande wake Daktari wazamu wa Hospitali ya Kivunge Makame Mdungi Makame amethibitisha kupokea mwili wa kijana huyo aliyefariki dunia baada ya kuzama katika mto, huko kilombero na amesema kifo chake kimesababishwa na kunywa maji mengi katika mto huo.
Aidha Daktari huyo alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuwadhibiti watoto wao kucheza karibu na mito na maeneo yaliyotuama maji ili kuepukana na majanga yanayoweza kujitokeza.
Matukio ya kuzama kwa watoto katika kijiji cha kilombero hutokea mara kwa mara hususani kipindi kama hichi cha mvua.
Na:Amina Omar Zanzibar24.

from Blogger http://ift.tt/2opkN06
via IFTTT