Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

Artificial Intelligence(AI), Gas Economy New Tanzania Priorities in 2024/25

Haya Ndiyo Madhara ya Kutisha ya Kufanya Ngono Kinyume na Maumbile..:;

Tokeo la picha la uchungu             
Ngono kinyume na maumbile au wengine husema Ngono kwa nyia ya haja kubwa, ni hali ya kingono ambayo muhusika huingiza uume katika njia ya haja kubwa kwa lengo la kufanya mapenzi kwa njia hiyo ili kujirishiza hisia zake.
Watu ambao wanajishughulisha na kushiriki katika ngono ya nia hii ya kinyume na maumbile wapo katika hatari kubwa ya kiafya, kwa sababu njia ya haja kubwa inazungukwa na mishipa/neva nyingi sana zipo eneo hilo ambalo kazi zake si maalumu kwa tengo la ngono kwa kuingiziwa kitu ambacho hakistahiri eneo hilo.
Ambapo kwa utafiti uliofanyika Nchini Tanzania uliohusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miakan 15 na kuendelea na iliyohusisha kada tofauti katika jamii kama wanafuzi, wafanyakazi, wahudumu wa baa, wauguzi, makahaba na kina mama wa majumbani katika maeneo tofauti. Watu waliojitokeza ni 903 wakiwemo pia wanaume walihusika katika tafiti hiyo.
Utafiti huo ulisema wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wamewahi kufanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambao ni sawa na asilimia 27 huku asilimia 73 ya waliohojiwa walidai kufahamu njia hiyo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, katika Utafiti huo ulifanywa na Irene Mremi kutoka Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Nchini Tanzania.
Inakadiriwa kuwa asilimia 90% ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao (mashoga) huwa wanajihusisha na ngono kinyume na maumbile.
JE, NGONO KINYUME NA MAUMBILE NI SALAMA?
HAPANA, Ngono kinyume na maumbile si salama kwa sababu ina madhara mengi kiafya kama yafuatavyo;
MOJA, Njia ya haja kubwa haina vilainishi/lubrication asilia kama jinsi Uke ulivyo.
Hivyo wakati wa tendo la ngono husasani wakati wa uingizaji wa uume huwa inasababisha kuchubuka kwa tisu/ngozi laini ndani ya njia ya haja kubwa hiyo, na hivyo kupelekea michubuko ambayo bacteria, virusi na hata vimelea vingine kuweza kupenyea wakati wa majeraha hayo ya michubuko na hivyo kuingia katika mfumo wa damu kupitia majeraha hayo.Hii inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa pamoja na VVU.
Tafiti zinaonyesha ya kuwa Ngono kwa Njia ya haja kubwa ipo katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa zaidi ya asilimia 30% kuliko watu wanaotumia njia ngono kwa njia ya Uke.
Vile vile mtu anakuwa katika hatari kubwa ya kupata virusi vya human papillomavirus (HPV ) ambavyo huweza kumpelekea mtu anayejihusisha na ngono kinyume na maumbile kupata muwasho katika eneo hilo la haja kubwa na hata kupelekea kupata kansa.
PILI, Tishu ndani ya njia ya haja kubwa, haijakingwa na kulindwa kwa ngozi ngumu kama ilivyo sehemu za nje za mwili. Tishu zote za nje ya miili yetu zina ngozi ambayo ni seli zilizokufa ambazo hutusaidia kutukinga dhidi ya maabukizi ya vimelea na vile vile hutulinda na vitu tofauti katika mazingira.
Hivyo ndani ya njia ya haja kubwa hakujakingwa na ulizi huo wa asili wa seli hizo ili kuweza kuhimili, hivyo kuifanya iwe katika hatari kubwa ya kusuguliwa na hivyo kuchanika ambayo hupekea kusababisha maambukizi kuwa rahisi kutokea.
Pia ngozi ndani ya njia ya haja kubwa iko tofauti na ile ya ukeni ambapo ngozi ya ukeni huweza kuhimili ile misuguano pasipo kuweza kusababisha michumbuko kwa sababu ya vilainishi asili vinavyoatikana ndian ya uke na gozi husika.
TATU, Njia ya haya kubwa ni Maalumu kupitisha Kinyesi tu.
Kwa jinsi ambavyo njia hii imeundwa ama kutengenezwa ni maalumu kwa kuhimili na kupitisha kinyeshi tu na si vinginevyo.
Njia ya haja kubwa imezungukwa na kama misuli mfano wa ringi ama kwa kitaalamu huitwa (Anal sphincter) ambayo kazi yake ni kukaza eneo hilo kabla na baada ya kujisaidia tu.
Kipindi ambapo misuli hiyo (anal sphincter)imekazwa ama kubwa kwa kuingiziwa kitu kingine kigumu huweza kusababisha maumivu makali kwa muhusika.
Panapoendelea kuwa na mrudio wa mara kwa mara wa ufanyaji wa Ngono kwa njia hii ya haja kubwa ama kinyume na maumbile hufanya misuli hiyo ya njia ya haja kubwa kuwa dhaifu ama kulegea na isiwe na uwezo tena wakukaza kama kazi yake inavyotakiwa kufanya. Na hivyo kuwa vigumu kuweza kuzuia kinyesi kuweza kupita mpaka utapokuwa tayari kuweza kukitoa hivyo kusababisha utokaji ovyo wa kinyesi.
NNE, Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi.
Njia ya haja kubwa imejaa bacteria wengi sana tofauti na Ukeni kulivyo hata kama wapenzi hawana maambukizi yeyote ya zinaa au ugonjwa wowote bacteria huwa wapo tu eneo hilo na hawa ni bacteria wa kawaida (Normal flora).
Mtu anapokuwa naingiza uume ndani ya njia ya haja kuwa anakuwa anaingiza vimelea vingine vya bacteria katika eneo hilo na wanapokutana na wale bacteria wengine waliopo katika eneo hilo husababisha madhara.
Pia pale unapohamisha uume toka katika njia ya haja kubwa na kupeleka katika Njia ya Uke badi bacteria hao utawapeleka katika eneo Uke ambapo Njia ya haja kubwa inakuwa na bacteria wengi na hivyo kupelekea maambukizi ukeni na pia maambukizi katika njia mkojo.
Ngono kwa njia ya haja kubwa inaweza kusababisha madhara mengine kwa afya ya watu wanaojihusisha na Njia hii ya ngono na wanaweza kupata madhaara kama haya yafuatayo,
Pale mdomo unapogusana na njia ya haja kubwa au kugusa uume uliotoka kwenye njia ya haja kuwa kwa mdomo kunaweza kupelekea kupata kwa wote mtu na mpenzi wake kuwa katika hatari ya kupataa magonjwa ya HEPATITIS C, HERPES/ malengelenge, kupata virusi vya human papillomavirus (HPV) na maambukizo mengine.
Hata hivyo, majeraha makubwa wakati wa ngono kwa njia ya haja kubwa mara nyingine ingawa sio kila mara hali hii kutokea inaweza kupelekea Damu kuvuja kwa ndani (hemorrhoids) baada ya tendo hilo kufanyika ambalo inaweza kusababisha au kupasuka ama kuchanika kwa misuli/nyama ndani ya njia ya haya kubwa kwa sababu ya msuguano mkali na muda mwingine hupelekea kuweza kutoboka kwa utumbo mpana(colon) hii huweza kwa ni tukio la hatari zaidi ambalo huhitaji msaada wa kitabibu haraka kwa matibabu na hata kufanyiwa upasuaji zaidi na hata kupoteza maisha kunaweza kutokea.
TANO, pia kwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao kushindwa kuhimili kukaza kwakati wa kusukuma mtoto na hivyo inaweza kupelekea utokaji wa kinyesi wakati wa kusukuma mtoto. jambo ambalo huleta tabu kwa wahudumu wa afya kwa kutumia muda mwigi kuwahudumia.
Njia pekee ya kuepuka kabisa hatari hizo za ngono kinyume na maumbile ni kuacha kabisa ngono kwa njia hiyo ya haja kubwa.
shiriki katika ngono kwa njia ya kawaida na ikibidi kwa kutumia kondomu ili kujilinda dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Kuepuka kuingiza uume ndani ya uke na kisha mdomoni ikiwa uume ulikuwa umeingizwa katika njia ya haja kubwa.
Ikiwa umepata michubuko na kutoka damu baada ya ngono ama vidonda karibia na njia ya haja kubwa na hata katika maeneo ya uke basi onana na daktari wako haraka iwezekanavyo ili upatiwe tiba hii iakusaidi kuzuia maambukizi ya vimelea katika eneo la jeraha.
MADHARA ANAYOWEZA KUYAPATA MWANAUME ANAYEPENDA KUJIHUSISHA NA MCHEZO HUU WA NGONO NI KAMA IFUATAVYO;
KWANZA, Kunauwezekano wa Njia ya haja ndogo kuziba kiasi au kuziba kabisa kwa sababu ya vimelea kuingia na kuziba ama kuingia kwa kinyesi katika njia ya haja ndogo hivyo kukuweka katika wakati mgumu utapohitaji kujisaidia haja ndogo.
PILI, unaweza kupata magonjwa ya saratani(kansa) ya tezi tezi Prostate gland.
TATU, Maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa sababu kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata maabukizi tofauti na kwenye njia ya Uke hii ni kutokana na kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata michubuko kiurahisi.
NNE, Kuathirika kisaikolojia hivyo mhusika kuandamwa na msongo wa mawazo kila wakati kujutia tendo hili baya.
Nina imanai ndugu msomaji wa makala hii umeweza kuona madhara mabaya sana ya tabia hii mbaya. Inawezekana umezoea mchezo huo wa kuwaingilia wenzako ama kuingiliwa kwa namna hiyo na kuona raha lakini umeziona hasara zake, amabazo kwa hakika kama wewe ni mmoja wao, unatakiwa kuacha mara moja kwa vile mwisho wake ni majuto na mateso.
Jiepushe kuiga mambo bila kujua hasara zake, pia usimtie mwenzako majaribu kwa kumlazimisha kufanya kitendo hiki na wanaume kwa kigezo cha kuachwa kwa lengo la kuwaingilia kinyume na maumbile kwa kuwatishia kuwaacha kama watakataa.
Kipi bora kuharibiwa ama kuachwa? Jibu unalo mhusika!!
Kumbuka baada ya kuharibiwa thamani yako inashuka mbele ya jamii. Kasha kupelekea kuingia katika msongo wa mawazo na mateso ya ugonjwa ama magonjwa utakayoyapata baada ya kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile.
UKWELI MCHEZO HUU UMEWAATHIRI SANA WANAWAKE NA WANAUME AMBAO WENGI WANAUJUTIA.
JIEPUSHE NA NGONO KINYUME NA MAUMBILE!!!!!    









COMMENT AND SHARE...................................!!!!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube