Tz Town Tv: Miundombinu ya Utalii Iimarishwe Nyanda za Juu Kusini

Post a Comment
KUTO imarisha miundominu ya kitalii mkoani Njombe kuna ikosesha fedha nyingi za kigeni serikali kwa kuwa watalii hawatembelei kwa wingi katika vivutio vilivyoko mikoa ya nyanda za juu kusini vikiwevyo vya Kitulo kwenye bustani ya maua ambayo ina ndege wengi wa aina tofauti.

Hayo yanabainishwa na wakazi wa Njombe ambao wanasema kuwa kuto kuwapo kwa miundombinu wezeshi kinakwamisha watalii kuingia katika mkoa huo huku uwanja wa ndege na barabara za kufika katika maeneo ya kitalii wakizitaja.

Wakizungumzia kwa nyakati tofauti masuala ya kitalii mkoani Njombe kulinganisha na mikoa ya Kaskazini wanasema kuwa miundumbinu ikiwa vizuri serikali itaingiza fedha nyingi za kigeni.

Aidha serikali nayo inasema ina mpango wa kuhakikisha kuwa mazingira ya utalii unakuwa katika mikoa ya nyanda za juu kusini ambapo tayari kwa kutoa elimu kwa watakao wapokea watalii kwenye nyumba za kulala wageni.

Mkuu wa mkoa anafunga mkutano wa elimu kwa wahotelia ulioandaliwa na Spanest ambapo anasema kuwa Mahotelia wanatakiwa kuwa na ukarimu ambao utavutia watalii na kufahami vivutia kitu ambacho kimefanyika kwa siku tatu.

Wanufaika wa elimu hiyo wanasema kuwa sasa wamepanuka kimawazo na wapo tayari kupokea watalii na kuwaeleza vivutio vya utalii kwa na kuwaeliza watalii vovutio vya mkoani Njombe.

TAZAMA WANANCHI WAKIISHAURI SERIKALI KUHUSU UTALII............................

Related Posts

Post a Comment