Mambo haya ya ajabu kuhusu Steve Jobs na Apple yatakushangaza

1. Steve Jobs hakuwahi kujuhusisha na uundwaji wa kiufundi wa bidhaa yoyote kutoka Apple



Steve Jobs maisha yake yote ya kufanya kazi Apple hakuwahi kuandika code wala kuunda kifaa chochote kile katika kampuni hiyo, kompyuta ya kwanza ya Apple ilitengenezwa na Steve Woz yeye alifanya kuitanganza tu.

Jamaa alikuwa kweli wa ajabu!

2. Hauruhusiwi kuvuta sigara ukiwa unatumia kompyuta za Apple



Kibali cha matumizi kutoka kwa Apple kinamzuia mtumiaji wa kompyuta zao kuweza kuvuta sigara wakati akitumia.

Ushafahamu?

3. Alipozikwa Steve Jobs hakuna jiwe la kumbukumbu



Mahala ulipo lazwa mwili wa steve jobs hakuna jiwe la kumbukumbu kutokana na mtaalamu huyo kupenda kuweka usiri katika mambo yake mengi wakati alipokuwa hai.

4. Apple wanaingiza dola 300,000 kila dakika



Kampuni ya Apple wanaingiza pesa nyingi kuliko hata wewe kwa mwaka mzima kutokana na mauzo ambayo yanafanyika duniani kote kila baada ya sekunde 60 wanaingiza zaidi ya milioni 600 za kitanzania.

Natamani ningekuwa nafanya kazi Apple.

5. Kupata kazi Apple sio jambo rahisi



Kuna uwezekano mkubwa wa kupata nafasi ya masomo katika chuo kikuu cha Harvard ambacho nafasi ya kusoma hapo hua ni ngumu sana kuipata, Kuliko kupata kazi katika stoo za Apple.

6. Steve Jobs alikuwa na tatizo la Dyslexic



Dyslexic ni tatizo ambalo mtu anakuwa anapata shida kwenye kusoma na kuandika ambapo husababishwa na ubongo kushindwa kutofautisha tarakimu. Ila kama mwenyezi mungu akikupa mapungufu katika jambo fulani, lazima atakupa uwezo wa juu katika jambo jingine ili kuziba pengo katika udhaifu uliokuwa nao.

7. Steve Jobs aliasiliwa



Baba yake halisi alikuwa ni mhamiaji kutoka nchini Syria aliyefahamika kwa jina la Abdulfattah Jandal ambaye alikutana na mama yake steve jobs Joanne Schieble wakati akifundisha huko Wisconsin nchini Marekani.

8. Vioo vya ipad vinatengenezwa na Samsung



Licha ya kuwa washindani wakubwa katika soko la vifaa vya kidigitali lakini kampuni ya Apple wanaagizia vioo vya ipad vinavyofahamika kama ipad retina display kutoka kampuni ya Samsung.

9. Steve Jobs alikataa kuwekewa ini



Miaka miwili kabla ya kufariki mkurugenzi mtendaji mkuu wa Apple sasa Tim Cook alijitolea ini lake ili awekewe steve jobs ambaye alikuwa anasumbuliwa na kansa, steve jobs alikataa jambo hilo akiona kama ingekuwa si vizuri.

10. Betri ya Apple Macbook ni kizuizi kizuri cha risasi.



Betri ya Apple Macbook inaweza kukusaidia dhidi ya risasi, Imetengenezwa na matirio ambazo ni ngumu kuweza pitisha risasi kwa urahisi.

ANGALIA VIDEO CHIDEO

Related Posts

Post a Comment