Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

Artificial Intelligence(AI), Gas Economy New Tanzania Priorities in 2024/25

Magonjwa ya Zinaa(Ngono ): Mambo Muhimu Wanayopaswa Vijana Kufahamu..:;

         
Utangulizi:
Magonjwa ya ngono ni magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya tendo la kujamiiana na mtu aliyeambukizwa magonjwa hayo bila kutumia kondom. Magonjwa haya  huweza kuwa-pata watu wa rika na jinsi zote hususani wale walio katika umri wa kuzaa (kati ya miaka 15-49).

Vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24 wanawakilisha moja ya tatu (1/3) ya idadi ya wakazi wote wa  Tanzania. Kundi hili liko katika hatari zaidi ya maambukizi  ya magon-jwa ya ngono kwa kuwa  wanapobalehe wanapata hisia za kupenda  na  pia  hamu  ya  kufanya  tendo  la  kujamiiana hujitokeza kwa nguvu. Hali hii huchochewa na vichocheo /homoni   vilivyomo mwilini ambavyo katika kupanda na kushuka husababisha hisia za kufanya tendo la kujamiiana. Hivyo basi,   ikiwa watakosa ufahamu wa kutosha kuhusu milli yao wanaweza  kujiingiza  katika tabia hatarishi  za kujamiiana bila kondomu na mwenzi zaidi ya mmoja.
Aina za magonjwa ya ngono:
Kuna  aina  mbalimbali  za  magonjwa  ya  ngono  ambayo yamegawanywa katika makundi kutokana na dalili zake kama ifuatavyo:
• Magonjwa yenye dalili za kutokwa na usaha au
majimaji sehemu za siri (ukeni na uumeni) ambayo ni Kisonono,Trikomonas na Kandida.
• Magonjwa yenye dalili za kutokwa na vidonda
ambayo ni Kaswende, Pangusa na Malengelenge sehemu za siri.
• Magonjwa yenye dalili za kutokwa na uvimbe
ambayo ni Mitoki, Pangusa na Malengelenge sehemu za siri.

Ieleweke kwamba, mtu anaweza kuwa na zaidi ya ugonjwa mmoja wa ngono kwa wakati mmoja. Kujitokeza kwa dalili za ugonjwa wa ngono hutegemea aina ya ugonjwa, jinsi na kinga ya mwili. Hata hivyo, baadhi ya watu hawaonyeshi dalili yoyote. Asilimia 10-15 ya wanaume na asilimia 60-70 ya wanawake  wenye  kisonono  hawaonyeshi  dalili  yoyote Hivyo basi, ni muhimu kijana unapoelezwa na mwenzi wako uliyefanya nae tendo la kujamiiana kwamba ameambukizwa ugonjwa wa ngono   usisite kwenda kituo cha huduma ya afya kwa uchunguzi na tiba hata kama huna dalili.
Dalili za magonjwa ya ngono:
Kijana uonapo dalili moja, au zaidi kati ya hizi zifuatazo nenda kwenye kituo cha huduma ya afya kwa uchunguzi;
Kwa kijana wa kike
• Maumivu chini ya kitovu
• Kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya
sehemu za siri (angalia picha)
•   Kuwashwa sehemu za siri
•   Vidonda na vipele sehemu za siri, mdomoni na sehemu nyingine za mwili

•   Maumivu wakati wa kujamiiana
•   Kuvimba mitoki
•   Kuota sundosundo sehemu za siri
•   Kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na muwasho au maumivu
Kwa kijana wa kiume:
•   Maumivu makali sehemu za siri wakati wa kukojoa
•   Kutokwa na usaha sehemu za siri
•   Vidonda sehemu za siri (angalia picha) Vidonda sehemu za mdomoni (angalia picha) Kuvimba mitoki
•   Kupata malengelenge

•   Kuota sundosundo (warts) sehemu za siri
Baadhi  ya  tabia  ambazo  zinaweza  kuchochea kupata maambukizi ya magonjwa ya ngono kwa urahisi zaidi:
•   Kujamiiana bila kondomu-vijana wengi hukosa
ujasiri wa kusisitiza matumizi ya kondomu kwa kuhofia kuachwa na wenzi wao
•  Kujihusisha na ukahaba
•  Kujamiina na wapenzi wengi
•  Kunyonyana sehemu za siri-kwa kuwa vimelea vya magonjwa ya ngono vinapatikana kwenye majimaji ya sehemu za siri ni rahisi mtu mwenye maambukizi ya magonjwa ya ngono kumwambukiza mwenzi
wakati wa kunyonyana.
•  Kunyonyana ndimi (kula denda)-baadhi ya vimelea vya magonjwa ya ngono hupatikana mdomoni
(Kisonono, Kaswende naVirusi vya UKIMWI) hivyo
huambukiza kupitia kunyonyana ndimi ikiwa mmojawapo ana maambukizi.

•  Woga wa vijana wa kike kuwashawishi vijana wa
kiume kutumia kondom wakati wa kujamiiana kwa sababu ya mfumo dume.
•  Kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazosababisha
kufanya ngono bila mpangilio, kwa mfano; makundi yanayoenda ufukweni, kuangalia filamu za ngono au kushiriki kwenye ngoma za jadi zinazochezwa
usiku kucha, disko na matamasha
•  Tamaa ya kupata pesa pamoja na vitu vya thamani
kama simu za mikononi, magari kutoka kwa watu mbalimbali
•  Kuhusika na vitendo vya ubakaji
•  Utumiaji wa madawa ya kulevya au pombe ambayo
husababisha kijana kukosa ufahamu na hivyo kufanya ngono isiyo salama.
KUMBUKA:
Kuwa  mwangalifu  wakati  wote  iIi  usiweze  kutumbukia kwenye tabia hizo. Ikibidi kujamiiana tumia kondomu kwa usahihi
Athari za magonjwa ya ngono:
Magonjwa ya ngono yasipotibiwa  mapema na kwa usahihi huweza kuleta athari zifuatazo kwa mgonjwa;
Kwa kijana wa kike:
•   Kuziba kwa mirija ya uzazi ambako kunasababisha
aidha mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi au ugumba
•   Maambukizi katika mfuko wa uzazi
•   Kupata Magonjwa katika viungo muhimu mwilini •   •  •   Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
•   Kansa ya kizazi
•   Mabadiliko ya hedhi
•   UKIMWI
Kwa kijana wa kiume :
• Maambukizi katika kokwa za mbegu za uzazi
• Kuziba mirija inayopitisha mbegu za uzazi na kuleta
utasa
• Kupata matatizo ya kukojoa kwa sababu ya kuziba
njia ya mkojo.
• Kupata Magonjwa katika viungo muhimu mwilini
kama ubongo, moyo, na figo
• Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
• Kansa ya uume
• Kupungua nguvu za kiume
• UKIMWI
KUMBUKA:
Athari zote hizi zinaweza kuepukika iwapo magonjwa ya ngono  yatatibiwa  mapema  na  kwa  usahihi. Usiogope! Magonjwa ya ngono yanatibika

Mbinu za kupambana na Magonjwa ya ngono kwa vijana:
Ili kuepukana na maambukizi ya magonjwa ya ngono zingatia yafuatayo:
• Usifanye kitendo cha ngono kabisa
• Jiepushe kufanya tendo la kujamiiana katika umri
mdogo
• Jiepushe na ulevi na madawa ya kulevya
• Jiepushe na vitendo vya ubakaji
• Jihadhari na kupiga denda na mwenzi usiyejua hall
yake ya afya
• Jiepushe na vitendo vya kunyonya uume au uke wa
mwenza
• Tumia muda wako mwingi katika masomo, kazi za
mikono, michezo na sanaa
• Epuka vishawishi kama zawadi na lifti za magari
barabarani
• Epuka kukaa na mpenzi wako peke yenu hasa
nyakati za usiku
• Epuka makundi ya vijana walevi, wazururaji na
wavuta bangi au watumiaji wa madawa ya kulevya
• Ikiwa umeoa au kuolewa, kuwa mwaminifu kwa
mwezi wako katika tendo la kujamiiana.
Kinga dhidi ya Magonjwa ya Ngono
• Acha ngono kabisa katika umri mdogo
• Tumia kondomu ya kike au ya kiume kwa usahihi
kwa kila tendo la kujamiiana
Mambo muhimu ya kuzingatia ukipata maambukizi ya magonjwa ya ngono:
• Wahi kwenye kituo cha huduma ya afya kilicho
karibu nawe  kwa uchunguzi na matibabu sahihi
• Tumia dawa zote kwa kufuata maelekezo ya
mtaalam wa afya hata kama dalili za ugonjwa zimepotea
• Epuka kujinunulia dawa bila maelekezo ya mtaalam
wa afya
• Usifanye tendo la ngono mpaka utibiwe na kupona
kabisa
• Muarifu mwenzi wako mapema iii wote  mkapate
matibabu sahihi na ushauri nasaha
KUMBUKA:
Kuwepo kwa magonjwa ya ngono kunaongeza uwezekano wa   kuambukizwaVirusiVya UKIMWI .
Source Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP) S.L.P 11857, Dar es salaam, Simu: 2131213
Faksi: 2119833,Tovuti: www.nacp.go.tz        




COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube