Habari

Kardinali Pengo aongoza Maaskofu kuuaga mwili wa Askofu Castor Paul Msemwa

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameongoza waumini na Maaskofu katika kuuaga mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na Masasi Castor Paul Msemwa katika Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Picha:

Katibu wa Rais Ngusa Samike akiaga mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa iliyofanyika katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam


Baadhi ya Mapadri nao wakipita mbele kuaga mwili wa Marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na Masasi Castor Paul Msemwa mara baada ya Misa katika Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.


Jeneza lenye mwili wa marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na Masasi Castor Paul Msemwa likiwa limebebwa na Mapadri wakielekea ndani ya Kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.


Makamu wa rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Dodoma Beatus Kinyaiya akizungumza kabla ya kuaga mwili wa marehemu Askofu Mkuu wa Jimbo la Tunduru na Masasi Castor Paul Msemwa katika kanisa la Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Askofu Mhashamu Castory

Picha na Full Shangwe

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents