WAKANDARASI WATAKIWA KUHAKIKISHA UJENZI WA UMEME UNAKAMILIKA KWA WAKATI

WAKANDARASI wa ujenzi wa umeme kutoka Makambako hadi Songea wametakiwa na serikali kukamilisha mapema ujenzi huo ili kuondoa tatizo la kukatika mara kwa mara kwa umeme wilaya za mkoa wa Ruvuma.
            
Umeme huo unatarajiwa kufikia vijiji 120 vya mkoa wa Ruvuma chini ya mradi wa REA awamu ya tatu ambapo lengo la serikali ni kufikia wananchi wote mwaka 2025.


Akizungumza na wakandarasi wa mradi wa umeme wa REA kutoka Makambako Mpaka songea Naibu waziri wa nishati na madini Medard Kalemani amesema kuwa serikali inataka umeme huo kufikia Septemba mradi uwe umekamilika.


Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mrati mbele ya naibu waziri Meneja wa mradi Mhandisi. Didas Lyamuya amesema kuwa utekelezaji wa mradi umekuwa ukikumbana na changamoto mbalimbali ikiwepo kucheleweshwa kwa fedha kutoka serikali kuu.



Mradi huo sehemu ya kwanza ni ujenzi wa njia ya umeme kwa kilomita 250 kutoka Makambako mpaka Songea kwa msongo wa kilovoti 220  upanuzi wa kituo cha Makambako kilovoti 220 na ujenzi wa kituo kipya Madaba na Songea kwa kilovoti 220 ili kuwezesha usambazaji wa umeme.